Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Viwanda vya ndani kwa lengo la kulinda ajira kwa watanzania na uchumi wa nchi usipotee.


Waziri wa Viwanda na Biashara DKt. Selemani Jafo (Mb) amesema kuwa dhamira ya Serikali  nikulinda viwanda vya ndani kwa lengo la kulinda ajira kwa watanzania na uchumi wa nchi usipotee.

Dkt.Jafo amesema Serikali imekuja na Sera mpya ya uendelevu wa viwanda ya 2025 ambayo itazinduliwa hivi karibuni ikiwa na sehemu ya jukumu la kuanzisha mfuko wa maendeleo ya viwanda ambao utaweza ujenzi wa miundombunu katika maeneo ya viwanda kama vile maji ,barabara na umeme ili kusaidia tasnia ya viwanda kwenda mbele.

‎Dkt. Jafo ameeleza hayo wakati wa Mkutano wake wa majadiliano na Wamiliki wa Viwanda nchini uliondaliwa na Shirikisho la Wenye viwanda (Cti) Julai 15,2025 jijini Dar es salaam.

‎Dkt.Jafo ameeleza kuwa hivi sasa nchi imejipambanua katika uzalishaji wa bidhaa katika viwanda ikiwamo  bidhaa za mabati, nondo, vioo, n.k na hadi sasa nchi inakidhi mahitaji ya ndani na kuweza kuwa na akiba.

‎Aidha Dkt.Jafo amewaambia Wamiliki hao kuwa katika kipindi kijacho maeneo ambayo yamekuwa na changamoto serikali itaendela kuyalinda maeneo hayo ikiwamo uimarishwaji wa miundombinu.

‎Naye Mkurugenzi mtendaji wa shirikisho la Viwanda Tanzania CTI Leodegar Tenga, ameeleza kuwa mwaka huu ni mapendekezo 56 yamepita kati ya 80 ambapo ni asilimia 70% ya mapendekezo, jambo ambalo serikali inaonesha kuwa ingependa kupiga hatua katika sekta ya viwanda kwaajili ya umuhimu wa viwanda nchini.

‎Kwa upande wake mwenyekiti wa shirikisho la Viwanda Tanzania Hussein suphian ameishukuru serikali kwa kuendelea kuboresha mazingira ya ufanyaji Biashara nchini, aidha amebainisha kuwa kwa mujibu wa takwimu za mwaka 2024/25 sekta ya viwanda imekuwa kwa asilimia 4.8 ikilinganisha na ukuaji wa asilimia 4.3 katika mwaka 2023/24. lakini pia mchango katika pato la taifa umeongezeka kwa mwaka 2024 kwa asilimia 7.3 ukilinganisha kwa mwaka 2023 ilikuwa asilimia 7.1 na hata Idadi ya ajira zinazopatikana Katika sekta ya viwanda zinzongezeka inaonesha kuwa hadi sasa watu ambao wameajiriwa ni takribani laki 4 , ukilinganisha na watu takribani watu laki 3 na elfu 70.