Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tanzania ni nchi salama yenye amani na utulivu, mazingira yanayofaa kwa biashara na uwekezaji.


Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo (Mb) amewakaribisha wawekezaji kuwekeza nchini, akisisitiza kuwa Tanzania ni nchi salama yenye amani na utulivu, mazingira yanayofaa kwa biashara na uwekezaji.

Akizungumza Juni 14, 2025 jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa kampuni ya Khushi Motors Tanzania, Dkt. Jafo amesema serikali imeweka mazingira bora ya biashara na kuwataka wawekezaji kutumia mawakala wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) ili kuhakikisha bidhaa zinazoingia nchini zinakidhi viwango vya ubora vinavyotakiwa.

Aidha, ametoa wito kwa Watanzania kuwaunga mkono wawekezaji wanaoleta biashara ya magari nchini, akisema hatua hiyo itasaidia kuepusha changamoto ya kuagiza magari kutoka nje na kisha kupata bidhaa isiyokidhi mahitaji ya mnunuzi.

“Tuwape ushirikiano wanaokuja kuwekeza hapa nchini badala ya kukimbilia kununua magari nje bila uhakika na utakacholetewa, jambo ambalo limekuwa likisababisha hasara kwa Watanzania wengi,” Dkt. Jafo.