Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tanzania yapendekeza AGOA iongezwe muda zaidi ya 2025


Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imependekeza Mpango wa Ukuaji na Fursa wa Afrika (AGOA) iongezwe muda zaidi ya 2025, kwa kipindi cha muda cha angalau miaka 20.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Ashatu Kijaji, ametoa wito huo wakati akichangia mjadala kuhusu utekelezaji wa Mpango wa huo wa AGOA katika Mkutano ngazi ya Mawaziri wa Nchi zinazonufaika na Mpango wa AGOA Novemba 2, 2023 katika Kongamano la 20 la AGOA linalofanyika Johannesburg, Afrika Kusini kuanzia tarehe 2-4 Novemba 2023

Kijaji amesema kuwa kipindi cha muda mrefu zaidi kitasaidia utelezaji wa AGOA na kuchochea uwekezaji wa muda mrefu katika nchi za Afrika kuliko kipindi cha maka 10 ambacho hakiwezi kutoa matokeo chanya na makubwa kwa wawekezaji.

Pia alisisitiza haja ya kuruhusu AGOA iweze kkujumuisha nchi zote wanachama wa Makataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA ) na kuimarisha ushirikiano kati ya AGOA na AfCFTA ili kuunga mkono juhudi za ushirikiano wa kikanda ili kupanua wigo wa AGOA pamoja na kuzingatia masuala mengine muhimu kama vile Biashara ya Huduma.

Kuhusu vigezo vya kuingia AGOA, Kijaji amesema kwamba nchi ambazo zimefikia hadhi ya kipato cha juu hazipaswi kutolewa mara moja kutoka kwa programu za GSP na AGOA, kwani nchi nyingi hizi zinaendelea kupata shida za kiuchumi na ukosefu wa ajira.

Pia aliomba marekebisho ya ukaguzi wa vigezo au sofa za kujiunga AGOA kkufanyika kila baada ya mika mitatu (3) badala ya ukaguzi wa kila mwaka hilivyo sasa. Hii itajenga ujasiri na muda zaidi kwa wawekezaji kufanya tathmini na kuchukua hatua za kurekebisha panapohitajika.

Kijaji pia alitoa wito wa kuondolewa kwa mahitaji ya Visa ya Nguo ambayo huongeza mchakato na gharama za kufanya biashara chini ya AGOA.

Alisema kuwa haya ni baadhi ya masuala ambayo Tanzania iliona inapaswa kuzungumzia, lakini kwa ujumla nchi inasaidia mapendekezo yote na inaamini kuwa ikiwa yatazingatiwa, yataleta matokeo chanya na kiwango cha matumizi ya AGOA kitaongezeka.