Habari
Ujumbe wa Tanzania amekutana na Balozi wa Tanzania nchini Oman

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda ma Biashara Dkt.Hashil T. Abdallah akiongoza Ujumbe wa Tanzania amekutana na Balozi wa Tanzania nchini Oman Mhe. Balozi Fatma Abdallah na kufanya kikao cha maandalizi ya Ziara ya Waziri wa Viwanda na Biashara nchini humo, Kikao hicho kimefanyika Aprili 27,2024 Jijini Muscat-Oman.
Ziara hiyo itaanza Aprili 28 hadi 30, 2025 ambapo Katibu Mkuu Dkt.Abdallah atamwakilisha Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo ambapo mambo mbalimbali yatafanyika ikiwemo kujadili masuala ya biashara, viwanda, ushirikiano wa kidiplomasia na kutembelea maeneo mbalimbali ya Uwekezaji wa Viwanda nchini humo.
Aidha Dkt.Hashil pia ameongozana na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Dkt.Stephene Nindi, Mkurugenzi Mtendaji wa TCCIA Bw.Oscar Kissanga,Wakurugenzi na Maafisa waandamizi kutoka Wizara hizo na Sekta binafsi.
Edited · 4h