Habari
Ujumbe wa Tanzania katika Kongamano la Biashara kati ya Marekani na Africa (2025 U.S -Africa Business Summit) linalofanyika jijini Luanda, Angola
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Exaud Kigahe (Mb) ameongoza Ujumbe wa Tanzania katika Kongamano la Biashara kati ya Marekani na Africa (2025 U.S -Africa Business Summit) linalofanyika jijini Luanda, Angola tarehe 23-25 Juni, 2025. Kongamano hilo limefunguliwa na Rais wa Jamhuri ya Angola, Mhe. João Manuel Gonçalves Lourenço.
Aidha, Kongamano hilo limehudhuriwa na Marais Sita, Mawazari Wakuu watatu, Mawaziri, Naibu Mawaziri kutoka nchi za Afrika pamoja na wawekezaji na Wafanyabiashara kutoka Afrika na Marekani ambapo zaidi ya Makampuni 300 kutoka Marekani yameshiriki.
Mhe. Kigahe ameambatana na Naibu Katibu Mkuu wa wizara ya viwanda na Biashara Dkt.Suileman Serera, Mwakilishi wa Heshima wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Jamhuri ya Angola Mhe. Mbwana Mziray, Maafisa kutoka Wizara ya Viwanda na biashara, wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Maafisa wa Ubalozi wa Tanzania, nchini Zambia,TIC, EPZA.