Habari
WATANZANIA WAASWA KUWA NA UTAMADUNI WA KUTUMIA BIDHAA ZA TANZANIA

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt. Selemani Jafo (Mb) amewaasa Watanzania kuwa na utamaduni wa kupenda kutumia bidhaa zinazozalishwa nchini.
Amebainisha hayo wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli za uwekezaji wa kiwanda cha Cocacola Kwanza kwa lengo la kuona shughuli mbalimbali za uwekezaji unaofanywa na kiwanda hicho kilichopo eneo la Mikocheni jijini Dar es salaam Agosti 22, 2025.
Waziri Jafo amesema amefarijika kuona teknologia kubwa ya uzalishaji iliyowekezwa na kiwanda hicho jambo ambalo linachangia uzalishaji mkubwa wa bidhaa zinazoenda sokoni.
Aidha Dkt.Jafo amesema uwekezaji wa kiwanda hicho unaleta tija kubwa kiuchumi kupitia uuzaji wa bidhaa hizo na kutoa ajira za moja kwa moja kwa vijana zaidi ya mia tisa (900) jambo ambalo linasaidia kupunguza tatizo la upatikanaji wa ajira nchini.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda hicho Bwa.David Chait amesema kiwanda hicho kimekuwa msingi mkubwa katika biashara nchini Tanzania kwa kuajiri Watanzania wengi kutoka na uwekezaji uliofanyika.
Bw.Chait amesema kuwa katika kipindi cha miaka 30 ya kiwanda cha Cocacola Kwanza nchini Tanzania wamekuwa wakizalisha bidhaa zinazokidhi viwango vya ubora kwa ajili ya walaji wa bidhaa na kuzingatia usalama kazini wakati za shughuli za uzalishaji.