Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Kikao cha 46 cha Maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji


Katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji, Biashara na Viwanda wa Kenya, Bi. Regina A. Ombam akiongoza Kikao cha 46 cha Maandalizi ya Mkutano wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) ngazi ya Makatibu Wakuu Mei 29, 2025 jijini Arusha, ambapo mapendekezo hayo yatawasilishwa katika Mkutano ngazi ya Mawaziri unaofanyika Arusha Mei 30, 2025.
Mkutano huo unaojumuisha Nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki, unajadili taarifa mbalimbali za mkutano uliopita na namna bora ya kuendelea kuboresha mazingira ya Kibiashara na Uwekezaji.