Habari
SERIKALI INAHAMASISHA NA KUWEZESHA UANZISHAJI WA BIASHARA NDOGO

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah amewahamasisha Wajasiriamali nchini kuanzisha biashara mbalimbali kuanzia biashara ndogo sana, ndogo, kati na kubwa ili kuongeza Ajira, Pato la Taifa na kukuza uchumi wa Taifa.
Vile vile amesema Serikali itaendelea kulinda na kuendeleza biashara zote kuanzia biashara ndogo sana, ndogo, kati na kubwa ambazo zinazofuata sheria na kanuni za nchi.
Ameyasema hayo Agosti 22, 2025 wakati akifungua rasmi Mgahawa wa Rhapta Gahwat and Food Point ulipo Victoria Jijini Dar es salaam.
Aidha, Dkt. Abdallah amesema Wizara ya Viwanda na biashara inaendelea kusimamia Sera na Sheria za uanzishwaji wa viwanda na biashara na iko tayari kuwezesha uanzishaji wa biashara ndogo kupitia nyanja mbalimbali.
Naye Mmiliki wa Mgahawa wa Rhapta Gahwat and Food Point Sheikh Issa Othman Issa amesema kuzinduliwa kwa Mgahawa huo bora ambao pia una sehemu maalumu kwa ajili ya mikutano na mafunzo inatoa fursa kwa Watanzania wengine kufanya biashara zingine katika eneo hilo.
Mmoja wa Wageni waalikwa katika hafla hiyo Bw. Mbaraka Islam anesema kuanzishwa kwa mgahawa huo kunahamasisha Wajasiriamali wengine Kanisa biashara Kama hiyo pia Mgahawa huo utarahisisha ufanyaji mikutano mbalimbali kwa kuwa sehemu hiyo inafikika kirahisi kutoka sehemu nyingi jijini Dar es salaam.