Habari
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb.) akipokelewa na Viongozi mbalimbali
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb.) akipokelewa na Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah akiwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Dkt. Said Mzee, Kaimu Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo (DRC) Mhe. Brigedia Jenerali Abssolom Lyanga Shausi, Mkurugenzi Idara ya Biashara Uwekezaji na Sekta za Uzalishaji Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Benjamini Mwesiga, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Ushindani (FCC), Bw. William Erio pamoja na Wataalamu wengine mara alipowasili katika Ofisi za Ubalozi huo Aprili 14, 2025 kwa ajili ya kushiriki Mkutano wa 26 wa Eneo huru la Biashara Afrika wa Baraza la Mawaziri wa Biashara wa AfCFTA utakaofanyika tarehe 15/04/2025.