Habari
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Ridhiwani Kikwete Pamoja na viongozi wengine wakishiriki Maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa yaliyofanyika katika Uwanja wa Mnara wa Mashujaa uliopo Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma Julai 25, 2025
Maadhimisho hayo yameongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Mkuu wa Mkoa wa Morogoro
Mhe. Adam Malima
Tanzania huadhimisha Siku ya Kuwakumbuka Mashujaa waliopoteza maisha yao wakiutetea, kuupigania na kuulinda uhuru wa Tanzania kila ifikapo Julai 25 ya kila mwaka. Siku hii ya kuwakumbuka mashujaa huambatana na shughuli mbalimbali ikiwemo dua na sala maalum ya kuwaombea mashujaa waliopoteza maisha na kuiombea amani nchi kutoka kwa viongozi wa dini. Pamoja na hayo hufanyika gwaride maalum kwa ajili ya mashujaa wetu.