Habari
WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA YASHINNDA TUZO UTOAJI HUDUMA BORA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwakabidhi tuzo Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Exaud Kigahe (kulia) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah kwenye Kikao kazi cha Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Mashirika na Taasisi za Umma kinachofanyika katika Ukumbi wa Kimataifa wa Arusha (AICC) Agosti 24, 2025.
Wizara ya Viwanda na Biashara imepewa tuzo hiyo kwa kuwa Taasisi yake ya WRRB imeshinda nafasi ya pili kwa kutoa huduma kwa wananchi.