Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Idadi ya Viwanda nchini yaongezeka ndani ya miaka minne ya Rais Samia.


Idadi ya Viwanda nchini yaongezeka ndani ya miaka minne ya Rais Samia.


Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo (Mb) amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa mabadiliko makubwa aliyoyafanya katika sekta ya viwanda nchini.

Ameyasema hayo Februari 27, 2025 Mkoani Tanga katika hafla ya ufunguzi wa kiwanda cha saruji cha Maweni Limestone.

Dkt. Jafo ameeleza kuwa takwimu zinaonesha kwamba, katika kipindi cha mwaka 2019-2021, Tanzania ilikuwa na viwanda takribani 52,000, lakini chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia idadi ya viwanda imeongezeka na kufikia viwanda 80,179.

Aidha Dkt. Jafo amesema kuwa mabadiliko hayo ni matokeo ya juhudi za Dkt. Samia ambaye amekuwa akifanya kazi kubwa ya kutafuta na kuvutia wawekezaji kutoka nchi mbalimbali duniani na kuifanya Tanzania kuwa eneo salama la uwekezaji ambapo juhudi hizo zimepanua fursa ya ajira kwa vijana wa Kitanzania jambo ambalo ni muhimu katika kukuza uchumi wa nchi.

Kwa upande mwingine Dkt. Jafo amesisitiza umuhimu wa kuendeleza sekta ya viwanda kama njia mojawapo ya kupunguza tatizo la ajira nchini, huku akielezea jinsi viwanda vinavyosaidia katika kuajiri vijana na kutoa fursa za kimaisha kwa wananchi