Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Kamati ya kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) imefanya ziara ya kutembelea Mradi wa jengo la Makao Makuu ya Shirika la Viwango Tanzania(TBS)


Kamati ya kudumu ya Hesabu za Serikali (PAC) imefanya ziara ya kutembelea Mradi wa jengo la Makao Makuu ya Shirika la Viwango Tanzania(TBS) @tbs_viwango kwa lengo la kukagua fedha zilizotengwa kugharamia ujenzi huo zinatumika kikamilifu Machi 12,2024 Jijini Dodoma.

Katika ziara hiyo Kamati hiyo chini ya Mwenyekiti wake Mhe Naghenjwa Kaboyoka amesema kazi ya ujenzi wa jengo hilo ni nzuri kuanzia nje lakini pia asilimia ya ukamilikaji wa jengo na matumizi ya fedha iliyotumika yanaendana inaendana.

Aidha Kamati imetoa ushauri kwa baadhi ya mapungufu yaliyoonekana katika ujenzi wa jengo hilo na kuagiza uongozi wa Shirika hilo wanasimamia ipasavyo sheria, kanuni na taratibu za utekelezaji wa miradi na kuhakikisha Mkandarasi wa jengo hilo anafuata taratibu za mkataba uliowekwa ili jengo hilo kukamilika kwa wakati.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Viwango Tamzania Dkt.Ashura Katunzi amekiri kuwepo kwa changamoto ya Mkandarasi kuchelewesha ujenzi huku akiwa haidai Serikali kulingana na madai anayoleta na kuiahidi kamati kufanya maboresho kwwnye ujenzi kutokqna na mapungufu.

Aidha Dkt. Katunzi amesema ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti 2025 na mpaka sasa umefikia asilimia 72.