Habari
Sekta Binafsfi kushiriki Expo 2025 kikamilifu
Sekta Binafsfi kushiriki Expo 2025 kikamilifu
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Biashara katika Wizara ya Viwanda na Biashara, Bw. Sempeho Manongi, anesema kuwa ushiriki wa Tanzania katika Maonesho ya Expo 2025 Japan unatarajiwa kuleta manufaa makubwa kwa Taifa, hususan katika kuimarisha intelejensia ya kibiashara, uchumi, diplomasia na biashara kwa ujumla.
Akizungumza kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Viwanda na Biasharana waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Aprili 17, 2025 , Bwana Manongi amebainisha kuwa kupitia ushiriki huo, Tanzania itapata fursa ya kukuza uchumi kwa kusaini mikataba mbalimbali ya biashara na uwekezaji na kujenga ushirikiano na makampuni makubwa kutoka mataifa mbalimbali.
Aidha Bw. Manongi amefafanua kuwa Siku ya Taifa ya Tanzania katika maonesho hayo itakuwa Mei 25, ambapo Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anatarajiwa kuwa mgeni rasmi. Siku hiyo itahusisha mijadala ya uwekezaji nchini na kuhudhuriwa na washiriki zaidi ya 300 kutoka ndani na nje ya nchi.
Aidha, Mei 26 kutafanyika Kongamano kubwa la kibiashara litakalotoa fursa kwa wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania kukutana na makampuni makubwa kutoka Japan na nchi nyingine kwa ajili ya kutia saini hati za mikataba ya kibiashara na uwekezaji pamoja na wadau muhimu wa maendeleo.
Naye Mkurugenzi wa Mtandao wa Wanawake Wajasiriamali Tanzania (TWCC), Mwajuma Hamza, amewahimiza wanawake kujitokeza kwa wingi kujisajili na kushiriki katika Maonesho ya Kimataifa ya Expo 2025 yatakayofanyika nchini Japani.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Huduma wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI), Bi Neema Mhando, amesema kuwa maonesho hayo yatakuwa daraja kwa wazalishaji kujifunza mbinu mpya za uzalishaji, kupata masoko mapya nje ya Afrika na kupeleka bidhaa zilizochakatwa kwa ubora wa kimataifa.
Pia Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania, Bw. Hamis Luvende, ameipongeza Serikali kwa kuwashirikisha wafanyabiashara katika maonesho hayo, na wameahidi kushiriki kikamilifu, huki wakoaminj kwamba tutaweza kujifunza, kupata bidhaa na teknolojia mpya, pamoja na kufungua milango ya ushirikiano wa kibiashara kimataifa.