Habari
SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YAAZIMIA USHIRIKI WA KISHINDO MAONESHO YA EXPO 2025 OSAKA JAPAN.
SERIKALI YA MAPINDUZI ZANZIBAR YAAZIMIA USHIRIKI WA KISHINDO MAONESHO YA EXPO 2025 OSAKA JAPAN.
Katibu Mkuu wa Viwanda na Biashara Dkt Hashil T. Abdallah na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Dr. Said S. Mzee wameshiriki kikao kazi cha Makatibu Wakuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Wadau wa Sekta binafsi na kuongea na waandishi wa habari ambapo kwa pamoja wameazimia kuwa na ushiriki wa kishindo katika maonesho ya Biashara ya Dunia EXPO 2025 OSAKA, JAPAN.
Kupitia maonesho hayo ya Dunia Watanzania watapata fursa ya kukutana na wadau mbalimbali kutoka nchi zaidi ya 160 katika sekta za Utalii, Miundombinu, Sanaa, Sayansi na Teknolojia, Kilimo, Mifugo, Uvuvi na Uchumi wa Buluu, Afya, Lugha ya Kiswahili na Utamaduni, Nishati, na Uwekezaji." ameeleza Dr. Hashil.
Aidha Dr. Mzee amewasisitiza Watanzania kujisajili kwa wingi zaidi kupitia tovuti ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ambayo ni www.tantrade.go.tz ili kuongeza idadi ya washiriki kutoka Tanzania kwenye Maonesho hayo nchini Japan.
Maonesho haya ya Biashara ya Dunia EXPO 2025 Osaka Japan yanaratibiwa na TanTrade kwa kushirikiana na Ubalozi wa Tanzania nchini Japan.