Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Vijana wa sasa wanapaswa kupatiwa limu ya dini ili kuondokana na changamoto ya malezi.


Mbunge wa Jimbo la Kisarawe na Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo, ameeleza kuwa kwa vijana wa sasa wanapaswa kupatiwa limu ya dini ili kuondokana na changamoto ya malezi.

Amebainisha hayo Machi 29, 2025, mara baada ya kumalizika kwa Mashindano ya 12 ya Kuhifadhi Qur’aan Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani.

Aidha ametumia fursa hiyo kusisitiza umma wa Watanzania umuhimu wa kuendelea kuliombea taifa ili kuendelea kuwa na amani na utulivu pamoja na mshikamano.

Aidha, Dkt. Jafo ametumia fursa hiyo kuwapa Waislamu wote nchini salamu za Eid ambayo inatarajiwa kufanyika hivi karibuni kulingana na muandamo wa mwezi.