Habari
Trekta za URSUS Kufanyiwa Tathmini

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Ashatu Kijaji (Mb) amekutana na kufanya
mazungumzo na Timu ya kufanya Tathmini za aina zote za matrekta ya URSUS Oktoba 30,2023 jijini Dar es Salaam.
Aidha timu hiyo imeundwa chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara baada ya maelekezo ya Spika wa Bunge na maoni ya kamati ya Kudumu ya Bunge ya Tathmini ambayo itawezesha Serikali kuandaa mpango wa kushughulikia changamoto za matrekta hayo kulingana na makundi ya wakulima.