Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Tumieni fursa ya biashara ya soko huria la Jumuiya ya Kikanda ya Afrika mashariki EAC na SADEC kupeleka bidhaa zenu


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt Ashatu Kijaji(Mb) amewasihi wanawake wajasiriamali kutumia fursa ya biashara ya soko huria la Jumuiya ya Kikanda ya Afrika mashariki EAC na SADEC kupeleka bidhaa wanazozalisha.

Ni katika hatua za utekelezaji wa mkakati wa maendeleo endelevu, ajenda inayojadiliwa na jumuiya za kimataifa na kikanda kwa kusisitiza jamii kuwekeza kwa mwanamke kwa ustawi wa kiuchumi kwa familia na jamii.

Dkt. Kijaji amesema hayo Februari 24,2024 kwenye hafla ya jukwaa la wanawake wajasiriamali wa wakiislamu lililoandaliwa na taasisi ya wanawake wa Kiislamu LADIES IN ISLAMIC Jijini Dar es asalaam kutangaza milango ya fursa katika soko la Afrika.

Kuhusu mpango wa mikopo ya wajasiriamali inayotolewa katika ngazi ya halmashauri Kijaji wamewashauri wanawake kujitokeza na kuchukua mikopo hiyo isiyo na riba.

Nae Mkurugenzi Mtendaji wa LADIES IN ISLAMIC Sarha Azizi amewakumbusha wanawake kuwa pamoja na kupambania fursa za uchumi na wasisahau wajibu wao katika malezi.

Katika Jukwaa hilo Wajarimali kadhaa wametunukiwa tuzo za ujasiriamali na kuiomba Mamlaka ya maendeleo ya Biashara nchini TANTRADE iliyo chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara kupunguza gharama za viingilio kwenye maonesho ya biashara Sabasaba.