Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Uchumi wa Buluu uwe ni fursa ya kuendeleza biashara na kuwanufaisha wananchi walio wengi.


Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt.Selemani Jafo (Mb) amesema Uchumi wa Buluu uwe ni fursa ya kuendeleza biashara na kuwanufaisha wananchi walio wengi.

Dkt.Jafo amesema hayo wakati wa kikao cha Mawaziri cha kuwasilisha mpango kazi wa utekelezaji wa shughuli za Uchumi wa Buluu nchini kwa mwaka 2024/25 na 2025/26 Februari 13, 2025 jijini Dodoma.

Aidha, shughuli za Uchumi wa Buluu hapa nchini zinatekelezwa kwa sera, sheria, miongozo, mikakati na mipango ya kisekta ikiwemo, Uvuvi, Nishati, Uchukuzi, Maliasili na Utalii, Maji, Umwagiliaji, Viwanda na Biashara, Uhifadhi wa Mazingira, Madini, na Uwekezaji.

Kwa Tanzania, Uchumi wa Buluu unajumuisha shughuli za kiuchumi zilizoendelevu zinazohusiana na bahari, maziwa, mito, mabwawa, Maeneo Oevu na maji chini ya ardhi kwa manufaa ya jamii bila kuathiri mazingira.