Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

jumbe wa Tanzania amekutana na kuzungumza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Unit Endüstri Makina Tekstil Ambalaj Tarım İthalat İhracat limited ya Uturuki Bw. Mustafa Albayram


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt. Selemani Jafo (Mb) akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah, Balozi wa Tanzania Nchini Ethiopia Mhe. Innocent Shiyo na ujumbe wa Tanzania amekutana na kuzungumza na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya
Unit Endüstri Makina Tekstil Ambalaj Tarım İthalat İhracat limited ya Uturuki Bw. Mustafa Albayram wa kuhusu fursa za uwekezaji na ufanyaji biashara Tanzania.

Mazungumzo hayo yamefanyika katika Ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Ethiopia Novemba 8, 2024 ambapo Waziri Jafo amemukaribisha Mwekezaji huyo kuja kuwekeza na kufanya biashara nchini.