Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Uwezeshaji wa wanawake kiuchumi ni moja ya kipaumbele ili kuleta usawa katika Jamii nchini.


Waziri ya Meandeleo ya Jamii, na Makundi Maalum Dkt. Dorothy Gwajima (Mb) amesema uwezeshaji wa wanawake kiuchumi ni moja ya kipaumbele ili kuleta usawa katika Jamii nchini.

Ameyasema hayo Desemba 6, 2023 katika ufunguzi wa Kongamano la Pili la Wanawake la Biashara la AfCFTA  linalofanyika kuanzia tarehe 6-8 JNICC, Jijini Dar es salaaam 

 Aidha, Gwajima amemtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kama mpenda usawa na mchochea maendeleo kwa wanawake.

Hii ni pamoja na Rais Samia kupitia Serikali za Mitaa kutoa mitaji kwa mkopo isiyo na riba kwa wanawake na vijana ili kuwainua wanawake katika jamii.

Aidha, amewapongeza waandaji wa Kongamano la AfCFTA la Wanawake katika Biashara chini ya Mkataba wa Eneo Huru la Biashara Afrika (AfCFTA) 

"Nawapongeza kwa kuandaa Kongamano hili kwa ajili ya wanawake, hii inaonesha jinsi gani tupo tayari kwa maendeleo ya mwanawake wa Tanzania na Afrika kwa ujumla" Amesema  Dorothy Gwajima