Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Uzinduzi wa Kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha "Global Packaging (T) Limited"


Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, sehemu ya Viwanda Mhe. Dkt. Adelhelm J. Meru azindua Kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha "Global Packaging (T) Limited kilichopo katika eneo la viwanda la Tamko Kibaha, Mkoani Pwani. Kiwanda kitaanza uzalishaji ifikapo January 2017 na kitazalisha vifungashio mil. 16 kwa mwaka na kiwanda kinategemea kuajiri zaidi ya watu 110 katika awamu ya kwanza.