Habari
Wafanyabiashara wa Mkoa wa Singida kwa kuendelea kuwa na biashara za kipekee zinazokuza jina la Mkoa wa Singida na kujulikana zaidi.

Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe (Mb) amewapongeza Wafanyabiashara wa Mkoa wa Singida kwa kuendelea kuwa na biashara za kipekee zinazokuza jina la Mkoa wa Singida na kujulikana zaidi.
Mhe.Kigahe ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa bonanza la michezo la watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Singida lilofanyika Januari 4, 2025 katika viwanja vya 'Bombadia' mkoani Singida.
Kigahe amesema kuwa "Singida kuna jina kubwa la mafuta ya kula ya alzeti, kuku, asali, vitunguu na biashara za utalii".
Pamoja na fursa hizi, Wizara ya Viwanda na Biashara ipo msitari wa mbele wa kuendelea kutoa elimu ya Biashara kwa wananchi.
Naye Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah amesema kuwa njia hii ya bonanza la michezo inasaidia kuwakutanisha wananchi, Wafanyabiashara na watumishi wa Wizara ya Viwanda na Biashara na kurahisisha utatuzi wa changamoto za wananchi za kibiashara na viwanda.