Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Wahitimu katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kutumia Elimu waliyopata kuwa chachu katika uchumi wa Tanzania.


 

 

Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe (Mb) amewataka wahitimu katika Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kutumia Elimu waliyopata kuwa chachu katika uchumi wa Tanzania.

Mhe.Kigahe ameyasema hayo Novemba 30,2024 alipokuwa mgeni rasmi kwenye mahafali ya 59 ya CBE na ya 11 katika Kampasi ya Mbeya akimwakilisha Spika wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Tulia Ackson.

Akitoa hotuba yake kwa wahitimu hao Mhe. Kigahe ameeleza kuwa elimu waliyoipata chuoni hapo, ikawe chachu katika maisha yao na waitumie ili kuwasaidia kubadilisha uchumi wa Tanzania kupitia biashara hasa katika Ukanda wa Afrika Mashariki na kati.

Ameongeza kuwa wahitimu wanapaswa kutafasri maarifa waliyopata hapo chuoni kwa tija katika Dunia hii ambayo imebadilika ujasiliamari na uvumbuzi vimekuwa ufunguo wa mafanikio kwa vijana wengi.

Aidha, ameeleza kuwa Taifa la Tanzania linawategemea wahitimu hao ,hivyo ni jukumu lao kutumia fursa kwa kujifunza zaidi na kuwa wabunifu katika masuala ya ujasiliamari hasa matumizi ya teknolojia ya kisasa ikiwemo ufahamu wa masoko ya kimataifa.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Uongozi wa CBE Dkt.Kennedy Hosea ameeleza kuwa Chuo hicho kimeanza kutoa shahada za awali (Bachelor Degree) kwa program nne katika Kampasi ya Mbeya kuanzia mwaka wa Masomo 2024/2025 tofauti na hapo awali.

Ameeleza kuwa CBE nchini imeanza kutoa shahada za umahiri (Master Degrees ) kwa njia ya Mtandao ambayo imewezesha Watanzania wengi hasa waliopo maeneo ya pembezoni kupata Elimu bila kusafiri kwenda mbali.

Kwa upande wake Mkuu Chuo cha CBE Prof. Edda Lwoga amesema kuwa, CBE ina wanafuzi takribani elfu 20 huku katika Kampasi ya Mbeya pekee ikiwa na wanafunzi 1030 na vilevile ndio Chuo kikongwe kilichozalisha wataalam wengi sana waliobobea katika masuala ya biashara nchini.

Vilevile ameelezea majukumu makubwa yanayotekelezwa na Chuo hicho kuwa ni matatu ambayo ni.- kutoa eimu ya biashara ,kufanya tafiti mbalimbali zinazohisiana na mambo ya biashara na kutoa ushauri wa kitaalam