Habari
Wahitimu wa CBE waaswa kujiepusha na makundi hatarishi ya Madawa ya kulevya

Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashill Abdallah ametoa wito kwa wahitimu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) kujiepusha na tabia hatarishi , makundi yasiyofaa ikiwemo matumizi ya madawa ya kulevya.
Dkt. Hashill ametoa wito huo kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara (Mb) Dkt. Ashatu Kijaji wakati wa mahafali ya 58 Kampasi ya Mbeya katika Ukumbi wa Chuo cha Elimu ya Biashara CBE Iganzo-Mbeya tarehe 2 Desemba 2023.
"Wahitimu zingatieni yale yote mliyofundishwa na kuyafanyia kazi ili yalete manufaa,mnapaswa kuwa wabunifu katika kutumia maarifa mliyopata ili kukabiliana na changamoto mbalimbali na kujiepusha na makundi yasiyofaa na matumizi ya Madawa ya kulevya" Amesema Dkt.Abdallah.
Naye Mwenyekiti wa bodi ya uongozi wa CBE Prof. Wineaster Anderson ameeleza kuwa Kampasi ya CBE Mbeya imetimiza miaka 10 toka ilipoanzishwa mwaka 2013 na imefanikiwa kununua eneo jipya lililopo Iganzo lenye ukubwa wa hekari 54.9 na kujenga miundombinu ya majengo mapya ambayo yanayotumika kufundishia na kutoa huduma zingine katika Kampasi ya Mbeya.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha CBE Prof. Edda Tandi Lwoga katika hotuba ameeleza kuwa Chuo kinaadhumisha maafali ya 58 toka kianzishwa kwake 1965, yakiwa maafali 10 kwa Kampasi ya Mbeya ambapo ujumla ya wanafunzi 1008 kati ya 17205 wakitoka Kampasi ya Mbeya.
Aidha ameeleza kuwa katika Kampaso ya Mbeya CBE inatoa kozi mbalimbali kwa ngazi za Astashada, Stashahada na Shahada katika masomo ya Uhasibu, Uongozi wa Biashara, Masoko, Ununuzi na Metologia ya Viwango