Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Wajumbe wa kamati ya ujenzi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kutembelea chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC).


Wajumbe wa kamati ya ujenzi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kutembelea chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC). Wajumbe wa kamati ya Ujenzi wa Wizara ya Viwanda na Biashara wamepata fursa ya kutembelea Chuo cha Taifa cha Ulinzi (National Defense College - NDC) Kilichopo Kunduchi jijini Dar es salaam. Lengo la ziara hiyo ilikuwa kuona jengo la mafunzo na ofisi linalojengwa na Kampuni ya China State Construction Co Ltd ili kupata uelewa wa pamoja wa namna bora itakayosaidia ujenzi wa majengo ya Wizara ya Viwanda kuwa bora na ya kisasa.