Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt.Selemani Jafo(Mb) amesema wananchi 436 kati ya 595 tayari wamelipwa fidia kwa ajili ya kupisha utekelezaji wa Mradi wa Magadi Soda ya Engaruka uliopo wilayani Monduli mkoani Arusha.
Dkt. Jafo amebainisha hayo Februari 13, jijini Dodoma akihojiwa katika kipindi cha Morning Trumpet Azam Tv na kusema kuwa wananchi wa vijiji vya Engaruka Chini, Mbaash, Idonyonado na Irerendeni wamechukua fidia na wanaendelea kuchangamkia fursa mbalimbali za kibiashara kwa kuwekeza kwenye vitega uchumi.
Aidha, Serikali ya Tanzania kwa mara ya kwanza ilisaini mkataba wa uwekezaji Maganga Matitu wa uzalishaji wa chuma ambapo ni jambo kubwa sana kwani litafanya kupiga hatua kwa sababu Tanzania inafanya uzalishaji wa chuma lakini viwanda vya chuma vina changamoto mbalimbali za kimiundombinu.
Vilevile Dkt.Jafo amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ulipaji fidia ya sh. bilioni 15.4 katilka mradi wa Liganga na Mchuchuma baada ya kufanya tathmini na Bilioni 14.4 za mradi wa magadi soda ambayo ni malighafi ya viwanda vingi.
Dkt.Jafo pia amewataka Watanzania kuwa watulivu wakati Serikali ikiendelea kutafuta suluhisho la kudumu la soko la Kariakoo.