Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Wananchi wapewa rai kuacha kuchanganya mazao ili kutokuharibu au kupunguza thamani ya mazao


Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Dkt Selemani Jafo (Mb) ametoa rai kwa Watanzania kuacha kuchanganya mazao ili kutokuharibu au kupunguza thamani ya mazao hayo katika soko la kimataifa na kuharibu taswira ya Tanzania.

Aidha ameliagizza Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kuendelea kusimamia na kufuatilia ubora wa Mazao hayo yanayohifadhiwa na kuuzwa kupitia Mfumo wa Stakabadhi Ghalani na Wakala wa Vipimo (WMA) kuhakikisha mizani zote nchini zinapima mazao kwa usahihi

Ameyasema hayo Septemba 18, 2024 alipotembelea Ghala la Mpako linalotumia Mfumo wa Stakabadhi ghalani wakati wa Ziara Maalum Wilaya ya Liwale, Mkoa wa Lindi yenye lengo la kukagua utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo na kuongea na Wananchi wa Maeneo hayo ikiongozwa na Kauli Mbiu isemayo "Rais Samia na Maendeleo Wasikie na Waone" iliyoanza tarehe 17 - 21/09/2024 Mkoani humo.

Vilevile akiwa katika Ghala hilo amesema ameridhika na ujenzi wa wake na ameiagiza Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) ndani ya siku 20 kukaa kikao na Bodi ya Korosho ili kufanya tathimini ya siku ngapi zinafaa kutoa korosho gharani huku wakifanya utafiti wa kina kuhusu suala la unyaufu katika zao la Korosho ili kuhakikisha wananchi wanafaidika na mazao yao ya kilimo.

Aidha, katika ziara yake Wilayani humo amebainisha kuwa fedha zilizotolewa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa ajili ujenzi shule za sekondari na zahanati imetumika vizuri na miradi hiyo imejengwa katika kiwango kinachohitajika

Akiongea na Wananchi wa Liwale Dkt Jafo amesema Serikali ya Awamu ya Sita itaendele kutatua changamoto mbalimbali walizonazo ikiwemo kuweka mindominu wezesheshi ya barabara , maji na umeme ili kuhakikisha uchumi wa nchi hii inaongea na kukuza uchuma

Naye Mkuu wa Wilaya ya Liwale Mhe Goodluck Mlinga ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo Wilayani humo na kuahidi kuwa Wilaya yake itaendelea kusimamia Miradi hiyo kikamilifu.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB) Bw. Asangye Bangu amewashauri Wananchi wa Liwale kuendelea kutumia Mfumo wa Stakabadhi Ghalani unaowawezesha wakulima kuuza mazao hayo kwa bei n