Habari
Watanzania kutumia fursa za kusafirisha mazao na nyama katika Nchi ya Omani

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Selemani Jafo (Mb) amewaasa Watanzania kutumia fursa za kusafirisha mazao na nyama katika Nchi ya Omani kutokana na nchi hiyo kuwa uhitaji mkubwa wa vitu hivyo ambapo utachochea kuongeza pato la Taifa na mtu mmoja mmoja.
Ameyasema hayo katika hafla fupi ya kuadhimisha Miaka 54 ya Kisultani ya Taifa la Omani iliyofanyika Novemba 19,2024 katika ukumbi wa Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam.
Dkt.Jafo amesema Mataifa hayo mawili yamekuwa na uhusiano mzuri wa kidiplomasia na Biashara hususani katika biashara ya nyama na mazao ya kilimo, hivyo ni wakati sasa wa Watanzania kuchangamkia fursa hiyo.
Aidha .Waziri Jafo amesema hivi karibuni Mataifa hayo mawili yameanza makubaliano kwenye nyanja za usafirishaji ambapo itachochea shughuli za uchumi kwani mwanzoni mwa mwaka 2025 Shirika la ndege la Tanzania (ATCL) litaanza kutoa huduma za usafiri kutoka Tanzania kwenda Oman.
Nae Balozi wa Oman Nchini Mhe. Saud bin Hilal Alshaidani amesema kuwa Tanzania na Omani zina uhusiano ma Mashirikiano mazuri katika Masuala mbalimbali kama Biashara,diplomasia na tamaduni kwani kumekuwa na wafanyabiashara wengi wanaokwenda Oman na wa Oman kuja Tanzania.