Habari
Waziri KIgahe atoa rai kwa Taasisi za Serikali na Mashirika binafsi kutumia fursa ya Maonesho ya Biashara ya 10 ya Kimataifa Zanzibar

Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe ametoa rai kwa Taasisi za Serikali na Mashirika binafsi kutumia fursa ya Maonesho ya Biashara ya 10 ya Kimataifa Zanzibar kuonesha bidhaa zao ili zipate kujulikana nje ya Tanzana kuweza kupata soko hiyo ni kutokana na uwepo wa wageni wengi Zanzibar
Ameyasema hayo januari 11,2024 alipokuwa mgeni katika maonesho ya 10 ya biashara ya kimataifa Zanzibar (ZITF) katika viwanja vya maonesho fumba,Zanzibar.
Aidha amesema kuwa ni wajibu wa sasa kwa Wizara ya Maendeleo ya biashara Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ni kutumia eneo hilo jipya kwa shuguli za maonesho ya biashara kwa mwaka mzima ili kuhakikisha eneo hilo linaleta tija kwa wananchi na wafanyabishara kwani lina uwezo wa kuhudumia Zaidi ya watu 400.
Vilevile Mhe.kigahe Amewataka wazalishaji wa bidhaa za viwandani kuongeza thamani ya na ubora wa bidhaa zinazozalishwa hizo nchini ili kuweza kufikia viwango vya kimataifa na kuweza kupata soko nje ya Tanzania