Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Waziri Mkuuu amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara kuwahamasisha Wamiliki wa Viwanda na Wafanyabiashara kwa ujumla kuchangia Timu za Taifa.


Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah kuwahamasisha Wamiliki wa Viwanda na Wafanyabiashara kwa ujumla kuchangia Timu za Taifa.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo Januari 10, 2024 jijini Dar es Salam wakati akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kuongoza hafla ya Harambee ya kuchangia Timu za Taifa zinazoshindana michuano mbalimbali ya kimataifa jijini Dar es Salaam

Wakati akipokea agizo hilo Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah alisema Wizara yake itatekeleza agizo hilo kwa kuwahamasisha Wamiliki wa Viwanda na Wafanyabiashara kupitia vyama vyao ikiwemo Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) kuchangia Timu hizo ili ziweze kishiriki mashindano hayo.

Aidha, Dkt Abdallah alibainisha kuwa Wizara yake pamoja na Taasisi zilizochini yake imechangia kiasi cha shilingi milioni 25 kwa ajili ya kuziwezesha Timu za Taifa ikiwemo Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya wanaume "Taifa Stars " na Timu ya Taifa ya wanawake ya Mpira wa miguu “Twiga Stars” zilizofuzu kucheza mashindano ya AFCON yanayofanyika nchini Ivory Coast na Morrocco mwezi huu 2024