Habari
Waziri Prof. Kitila Mkumbo amekagua ukarabati wa Ofisi mpya za Wakala wa Usajili wa biashara na leseni (BRELA) unaotekelezwa na Construction Ltd

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Prof. Kitila Mkumbo amekagua ukaraba wa Ofisi mpya za Wakala wa Usajili wa biashara na leseni (BRELA) unaotekelezwa na Construction Ltd.
Utekelezaji wa mradi huo kwa sasa upo 81%, kazi zilizobaki ni kazi za nyongeza ambazo ni marekebisho ya mfumo wa zimamoto, Tehama na ukamilishaji wa masinki ya vyoo
Mkataba wa utekelezaji wa mradi ni miezi mitatu na utakamilika Juni 30,2021 na utakapokamilika utaondoa adha waliyonayo kwa sasa na kuepuka gharama za kulipa kodi ya pango.
Leo Aprili 21, 2021 Dar es salaam