Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) alitoa rai kwa Watumishi wote wa Taasisi za Umma


  • Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji (Mb.) alitoa rai kwa Watumishi wote wa Taasisi za Umma zinazohusika na utoaji wa leseni na vibali mbalimbali kwa Wafanyabiashara na Wawekezaji kutekeleza jukumu hilo kwa ufanisi bila kukwamisha biashara.

    Dkt. Kijaji ameyasema hayo Novemba 17, 2023 jijini Tanga wakati wa ufungaji wa Kongamano la Uwekezaji Biashara na Utalii la Mkoa wa Tanga lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa mkoa huo kuanzia Novemba 16, 2023.

    Aidha, Dkt. Kijaji aliwahimiza wawekezaji wa ndani na nje ya nchi kutumia fursa zilizopo katika Mkoa wa Tanga ikiwemo ikiwemo Biashara, kilimo, viwanda na utalii pamoja na
    uzalishaji wa bidhaa na huduma mbalimbali kwa ajili ya soko la ndani na la Kimataifa ili kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa mkoa huo na wa Taifa kwa ujumla.

    Dk. Kijaji pia alitoa rai kwa wawekezaji kushirikiana na Serikali katika kuongeza tija katika uzalishaji kwenye sekta zote ili kuleta Mafanikio ya jitihada za Serikali za ujenzi wa uchumi wa viwanda.

    Vilevile Dkt. Kijaji aliupongeza uongozi wa Mkoa wa Tanga kwa jitihada zinazofanywa katika kuvutia uwekezaji na kukuza biashara kwa lengo la kufikia malengo ya kujenga uchumi wa viwanda kwa kuwa

    Dkt Kijaji pia amebainisha kuwa Serikali inaendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini ili kuwavutia wawekezaji kwa kufuta na kupunguza kodi na tozo mbalimbali, pamoja na kuzuia zoezi la kufungwa kwa viwanda na shughuli za biashara kwa Taasisi za Udhibiti.

    Dkt. Kijaji pia alibainisha kuwa Wizara yake itaendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa Uongozi wa Mikoa yote ili kuhakikisha kwamba fursa nyingi za kiuchumi zilizopo kwenye sekta za Kilimo, Uvuvi, Maliasili, Madini, Mifugo, na Utalii zinatumika ipasavyo katika kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii katika Mikoa na Taifa kwa ujumla.