Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

HATUKUSUDII KUSAFIRISHA MAZAO GHAFI NJE YA NCHI-DKT.JAFO.


HATUKUSUDII KUSAFIRISHA MAZAO GHAFI NJE YA NCHI-DKT.JAFO.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo amesema kuwa Tanzania haikusudiii kusafirisha mazao ghafi nchi za nje kwani kwa kufanya hivyo ajira nyingi kwa vijana nchini zitapotea.

Dkt.Jafo amebainisha hayo katika Maonesho ya Nanenane 2o25 Kanda ya Kusini yaliyofanyika Katika Viwanja vya Ngongo Mkoani Lindi Agosti 8,2025 Mkoani Lindi.

Waziri Jafo amesema katika kulinda uchumi wa nchi amefurahishwa na Vyama vya Ushirika katika kuongeza thamani ya mazao kwa kuanzisha viwanda vya ubanguaji wa korosho ambapo itasaidia kuondokana na usafirishaji wa mazao ghafi.

Aidha Dkt.Jafo amewaasa Wananchi wa Lindi na Mtwara kuchukua mazuri waliojifunza katika Maonesho hayo na kuyafanyia kazi kwa vitendo ili kuongeza uchumi wao katika uzalishaji wa shughuli za uchumi katika maeneo yao na Taifa kwa ujumla.

Vilevile Dkt.Jafo amepzipongeza Taasisi za fedha hasa mabenki jinsi zinavyotoa huduma za elimu na mitaji kwa wakulima, uvuvi na mifugo ambayo riba yake ni chini ya 10%.

Aidha ametoa rai kwa Wataalamu mbalimbali kwa Serikali kuhakikisha wanakuwa mstari wa mbele katika kuwasaidia wakulima na wajasiariamali ma sio kuwa kikwazo kwenye shughuli zao za uchumi.

Pia Dkt.Jafo ameziagiza Taasisi za SIDO na TBS Mkoa wa Lindi na Mtwara kuhakikisha zinawalea wajasiriamali ili waweze kupata maendeleo ya uchumi kwenye nyanja za kilimo na uvuvi pamoja na wajasiliamali