Serikali imeendelea kuweka mazingira mazuri ya kuanzishwa Viwanda na Biashara nchini Tanzania.
Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe.Exaud Kigahe(Mb) Septemba 12, 2024 wakati wa ufunguzi rasmi wa Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ya 25 ya 'Buildexpo Afrika 2024' yanayofanyika Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Maonesho haya yanahusisha wamiliki wa Viwanda vikubwa barani Afrika na bidhaa wanazozalisha, teknolojia wanayoitumia pamoja na kutoa elimu ya ujasiriamali kwa kupitia bidhaa walizonazo katika mabanda ya maonesho.
Mhe. Kigahe ameongeza kuwa, Elimu ya kujifunza maendeleo haina mwisho. Hivyo amewasihi wananchi kuendelea kutembelea mabanda ya maonesho na kuchangamkia fursa ya kubadilishana mawazo na Habari, kuanzisha urafiki na ushirikiano na baadaye kupata watu ambao mnaweza kuungana kibiashara au kuanzisha ubia wa Viwanda vya pamoja au kuendeleza Biashara.