Habari
Wito kwa wanawake kushiriki kwenye mpango wa kuwezesha wanawake kunufaika na Soko Huru la Afrika
Waziri wa Viwanda na Biashara, Mh. Dkt. Selemani Saidi Jafo (Mb) ametoa wito kwa wanawake kushiriki kwenye mpango wa kuwezesha wanawake kunufaika na Soko Huru la Afrika kupitia programu ya Twende Sokoni Afrika.
Mh. Jafo ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa programu hiyo lililoandaliwa na Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC) na iliyofanyika hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam, leo Februari 15,2025.
Dkt. AKafi amesem Bara la Afrika linakua sana maana yake ni fursa kubwa ya kibiashara ambayo ikitumiwa vizuri italeta mafanikio makubwa sana hivyo ushiriki wa Watanzania ikiwa ni miongoni mwa nchi wanachama, unatanua wigo wa kuweza kufanya biashara katika nchi zisizopungua 54 na hii ni faraja kubwa sana na malengo ya programu hiyo ni kuipeleka nchi mbele.
Aidha, Dkt. Jafo ametoa wito kwa taasisi za kifedha zikiwemo benki kutoa mikopo ya riba nafuu kwa ajili ya wanawake wa mfano waliochaguliwa na TWCC ili kuuza bidhaa na kushindana katika masoko ya kikanda na kimataifa kupitia Soko Huru la Afrika (AfCFTA)
Vilevile Dkt. Jafo amesema kuanzishwa kwa programu hiyo ni sehemu ya jitihada za dhati zilizochukuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuifungua nchi kimataifa na hivyo kufanya mataifa mbalimbali kuiamini Tanzania.
Kwa upande wake Rais wa Chemba ya Wanawake Wafanyabiashara Tanzania (TWCC), CPA (T) Mercy Sila amemshukuru Mh. Dkt. Selemani Jafo kwa utayari wake wa kuwasikiliza na anaamini ataweza kufikisha mahitaji ya TWCC kwa Mh. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.