Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji yapata tuzo ya Uwasilishwaji bora wa taarifa ya fedha kwa mwaka 2015.


Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji yapata tuzo ya Uwasilishwaji bora wa taarifa ya fedha kwa mwaka 2015. Tuzo hizi ambazo hutolewa kila mwaka na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa mahesabu (NBAA), kwa tuzo zilizotolewa kwa taarifa za mwaka jana Wizara ya Viwanda imeshika nafasi ya kwanza katika Wizara zote kwa kuwa na taarifa bora na nzuri za mahesabu. Akipokea tuzo hiyo kutoka kwa Mhasibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bi. Rose Bandisa aliyeongozana na Wahasibu na Wakaguzi wa Ndani Katibu Mkuu wa wizara hiyo anayeshughulikia Viwanda Dr. Adelhelm Meru amesema kupata tuzo hiyo kumetokana na juhudi kubwa za kiutendaji kwa wahasibu, wakaguzi na watumishi wote katika kufuata misingi ya utumishi wa umma.