Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Wizara ya Viwanda na Biashara yawasilisha Bajeti ya Kiasi cha Sh.Bilioni 110.9 kwa Mwaka wa fedha 2024/2025 ili kutekeleza vipaumbele vikuu sita


Wizara ya Viwanda na Biashara imeliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha Bajeti ya Kiasi cha Sh.Bilioni 110.9 kwa Mwaka wa fedha 2024/2025 ili kutekeleza vipaumbele vikuu sita.

Akisoma makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2024/2025, Bungeni Mei 21, 2024 Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji(Mb) ametaja vipaumbele hivyo ikiwa ni pampja na kuendelea na utekelezaji wa miradi ya kielelezo na kimkakati; Kuimarisha uwezo wa uzalishaji viwandani na utoaji huduma kwa kuimarisha miundombinu na mazingira wezeshi. 

Pia, amesema vipaumbele vingine ni kuboresha mazingira ya uwekezaji viwandani na ufanyaji biashara, kuchochea maendeleo ya watu kwa kuboresha miradi na programu katika sekta za Kiuchumi na kijamii inayohusisha elimu na mafunzo ya ujuzi.

Dkt. Kijaji ametaja kipaumbele kingine ni kufanya intelijensia ya masoko ya bidhaa na huduma zinazozalishwa nchini kwenye masoko ya kimkakati na ya kimataifa na kuchochea ukuaji wa Sekta binafsi nchini.