Habari
Wizara ya Viwanda na Biashara inaendelea kutekeleza majukumu yake kama ilivyopangwa
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Exaud Kigahe (Mb) ashiriki Mkutano wa Washirika wa Maendeleo ya Sekta Binafsi na Maendeleo ya Biashara (PSD&T-DPG) ambao umelenga kujadili fursa za miradi mbalimbali ya kimkakati na kinara iliyoanzishwa chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara inatekelezwa, Agosti 15,2024 Jijini Dodoma.
Katika Mkutano huo Mhe.Kigahe amebainisha vipaumbele mbalimbali ambavyo washirika hao wameahidi kushirikiana na Wizara kuitekeleza ambayo ni pamoja na sekta ya viwanda,Biashara pamoja na Sera mbalimbali.
Aidha Mhe Kigahe amesema kuwa Wizara ya Viwanda na Biashara inaendelea kutekeleza majukumu yake kama ilivyopangwa kwa Mwaka wa Fedha 2024/2025 ili kujenga uchumi wa viwanda unaokuza mageuzi ya kiuchumi na kuhakikisha maendeleo ya watu.
Mkutano huo pia umeshirikisha Ofisi ya Rais Mipango na Uwekezaji ambapo Waziri wake Mhe.Prof.Kitila Mkumbo ameshiriki pamoja na baadhi ya Mabalozi.