Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

WMA na ZAWEMA zakubaliana


Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil T. Abdallah pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Masoko Zanzibar Ndugu. Ali Khamis Juma wameshuhidia kusainiwa kwa hati ya makubaliano ya mashirikiano (MoU) baina ya Wakala wa Vipimo Bara (WMA) na Zanzibar (ZAWEMA) ya kushirikiana katika maeneo mbalimbali ya kazi.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo tarehe 13.01.2024 baina ya Afisa Mtendaji Mkuu wa WMA Bi. Stella Kahwa na Mkurugenzi Mtendaji wa ZAWEMA Ndugu. Mohamed Simai katika kikao kazi Cha Watendaji Wakuu wa taasisi za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Bara na Zanzibar Dimani Fumba.

Mara baada ya hafla ya utiaji saini wa makubaliano hayo Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na BiasharaTanzania Bara Dkt.Hashil Abdallah alitoa maneno mafupi ya umuhimu wa makubaliano ya ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili.

Dkt.Abdallah amesema kuwa Ushirikiano baina ya taasisi hizo utasaidia kuinua ubora wa huduma za vioimo kwa kubadilishana uzoefu lakini pia kudumisha Muungano baina ya Tanzania na Zanzibar ambapo amesema ili kufika mbali ni lazima kwenda pamoja.

Kikao kazi hicho cha Wakuu wa Taasisi kilifunguliwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Exaud Kigahe (Mb)