Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

IKAO KAZI CHA MAANDALIZI EXPO2025 OSAKA JAPANI.


IKAO KAZI CHA MAANDALIZI EXPO2025 OSAKA JAPANI.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt Hashil Abdallah ameongoza kikao kazi cha maandalizi kuelekea Maonesho ya Biashara ya Dunia EXPO 2025 OSAKA yatayo fanyika Osaka Japani kuanzia tarehe 13 Aprili mpaka 13 Oktoba 2025.

Kupitia kikao kazi hicho kilichofanyika Aprili 3,2025 Jijini Dar es Salaam maswala mbalimbali yamejadiliwa kuhusu hali na hatua mbalimbali za maandalizi kwa lengo la kufanikisha maonesho hayo.

Kikao hicho kimefanyika katika Ofisi za TanTrade zilizopo katika kiwanja cha Mwl. Julius Nyerere barabara ya Kilwa Jijini Dar es Salaam.