Sekta Binafsi Zanzibar yahamasishwa kushiriki Maonesho EXPO 2025
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Aboud Suleiman Jumbe, ametoa rai kwa wananchi na wadau mbalimbali kutumia fursa hiyo kuitangaza Tanzania kiuchumi, kijamii na kimaendeleo.
Aidha, amewahamasisha Wadau wa biashara na utalii kishiriki kwa nguvu na kuwataka kutoa taarifa muhimu hususani taarifa za kidijitali ili kuhakikisha hakuna anayeachwa katika harakati hizi za kuitangaza nchi.
Dkt Jumbe ameyasema hayo Aprili 19, 2025 wakati wa akiongea na Waandishi wa Habari kuhusu Ushiriki wa Tanzania katika Maonesho Expo 2025, yatakayofanyika jijini Osaka, nchini Japani kuanzia Aprili 12 hadi Oktoba 13, 2025.
Aidha, ameeleza kuwa Tanzania itatumia fursa hiyo pia kutangaza kuwa mwenyeji wa Mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) kwa mwaka 2027. “Hii ni fursa nzuri kuvutia wadau, kwani mambo makuu ya kimkakati na kiuchumi yanahitaji kufanyika haraka,” aliongeza.
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Dkt. Hashil Abdallah amesema kuwa maonesho hayo yana faida kubwa si tu kwa dunia bali pia kwa Tanzania, ambayo tayari imethibitisha kushiriki na ni nafasi kwa wawekezaji na wafanyabiashara kutoka Tanzania kukutana na wenzao kutoka mataifa mengine.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Maendeleo ya Viwanda Dkt. Said S. Mzee amewasisitiza Watanzania kujisajili kwa wingi zaidi kupitia tovuti ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TanTrade) ambayo ni www.tantrade.go.tz ili kuongeza idadi ya washiriki kutoka Tanzania kwenye Maonesho hayo nchini Japan.
Naye Mkurugenzi Mtendaji, Jumuiya ya Wafanyabiashara Zanzibar (ZNCC), Ndugu Hamad Hamad amesema sekta binafsi ya Zanzibar itashiriki kupitia sekta mbalimbali zikiwemo utalii, uchumi wa buluu, viwanda, kilimo na nyinginezo. Pia wakulima wa mwani na majongoo ya baharini washiriki ili kuinua biashar