Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Dkt. Selemani Jafo, amesema jumla ya nchi 22 zimeshiriki Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), maarufu kama Sabasaba


Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Selemani Jafo, amesema jumla ya nchi 22 zimeshiriki Maonesho ya 49 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (DITF), maarufu kama Sabasaba, na kuleta wafanyabiashara kutoka nje ya nchi kushiriki katika tukio hilo muhimu na adhimu.

Amebainisha hayo wakati wa hafla ya ufunguzi rasmi wa maonesho hayo, Dkt. Jafo amesema maonesho ya Sabasaba yamekuwa yakivutia watu wa ndani na nje kila mwaka kwa kiwango kikubwa na huendelea kuboreshwa na hivyo kuvutia washiriki wapya kutoka ndani na nje ya nchi.
Kwa upande wa ndani, amesema washiriki kutoka taasisi mbalimbali nchini wamefikia zaidi ya elfu mbili, wakiwemo wafanyabiashara binafsi, taasisi za umma, idara na wizara za serikali.

Maonesho hayo yanatarajiwa kufikia tamati m Julai 13 mwaka huu, yakielezwa kuwa jukwaa muhimu la kukuza biashara, ubunifu, na ushirikiano wa wafanyabiashara wa ndani na wa kimataifa.