Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

BRELA, SIDO na Taasisi husika fikeni katika Ngazi za Halmashauri


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Exhaud Kigahe (Mb.) ameziagiza BRELA, SIDO na Taasisi husika kufika katika Ngazi za Halmashauri ili kuwawezesha Wafanyabiashara


Amesema hayo Octoba 3,2023 akiwa anafunga Kongamano la Biashara na Uwekezaji wilayani Pangani Jijini Tanga lililofanikiwa kuwakutanisha wafanyabishara mbalimbali mkoani Tanga.


Aidha, Kigahe amesema Serikali ya Awamu ya Sita inaendelea kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji na kuhakikisha sekta binafsi zinafanya
vizuri katika maendeleo ya biashara na uchumi


Aidha amewataka wafanyabiashara, Wadau wa Maendeleo na Wajasiliamali kuchangamkia Fursa za utalii, kilimo, ufugaji na chumi wa bluu katika wilaya ya Pangani


Vilevile, Kigahe amesema ni wakati sasa thamani ya Malighafi nchini iongezeke iwe maradufu na nchi iwe inazalisha bidhaa zilizokamilika ili ziweze kuingia
katika Soko Huru la Biashara Afrika na Masoko mengine ndani na nje ya Afrika


Vilele amempongezaa Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi Zainab Issah kwa maandalizi ya Kongamano hiloo nakua Mkuu wa Wilaya wa Kwanza Nchini  Kuaanda"Pangani Royal tour" itakayofungua milango katika Vivutio mbali mbali ikiwemo Hifadhi ya Saadani, Zao La Mwani, Uchumi wa Bluu, Kilimo na  Ufugaji


Naye Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mhe Zainab Issah ameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuifungulia maendeleo Pangani kwa ujenzi wa barabara Tanga-Pangani-Saadani-Bagamoyo, Daraja la mto Pangani na Miradi mbali mbali ya Maendeleo ili kuweza kuhamasisha uwekezaji na muingiliano
wakibiashara ndani na nje ya nchi.