Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

SERIKALI KUENDELEA KUIWEZESHA SEKTA BINAFSI KUKUZA SEKTA YA VIWANDA


Serikali imeahidi kuendelea kuiwezesha sekta binafsi kwa kuweka mazingira bora ya ufanyaji biashara na wekezaji ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kuhamasisha ushiriki wa sekta binafsi katika kukuza sekta ya viwanda na biashara na uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Judith Kapinga (Mb), Juni 03, 2026 alipokutana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Saruji ya Twiga Bw. Alfonso Velez katika Ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuendeleza na kuimarisha ushirikiano.

Aidha, amesema Serikali itaendelea kuimarisha ushirikiano na sekta binafsi ili kuongeza uwekezaji, ajira na maendeleo ya viwanda nchini pamoja na kutatua changamoto zinazojitokeza.

Naye Mkurugenzi wa Twiga Cement, Bw. Alfonso Velez, amesema Kampuni hiyo imejipanga kuwekeza zaidi ili kuendelea na upanuzi wa Kiwanda hicho kwa ajili ya kuboresha mifumo ya uzalishaji kwa ufanisi.