Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Dkt.Jafo ameishukuru Jumuiya ya wafanyabiashara kwa ushirikiano na uvumilivu mkubwa


 

 

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Dkt.Selemani Jafo (Mb) ameendelea kutoa Pongezi kwa vyombo vya ulinzi na Usalama na vikosi vya uokoaji pamoja na wafanyabiashara kwa ujumla kwa ushirikiano mkubwa wanaouonesha katika shughuli za uokoaji.

Ameyasema hayo Novemba 17,2024 aliposhiriki katika zoezi la uokoaji kufuatia kuanguka kwa ghorofa la Biashara Kariakoo iliyotokea Novemba 16,2024 Jijini Dar es Salaam.

Dkt.Jafo ameishukuru Jumuiya ya wafanyabiashara kwa ushirikiano na uvumilivu mkubwa katika kipindi kigumu kwani kilichotokea ni moja ya changamoto na imani yake zoezi la uokoaji litakapokamilika shughuli za biashara zitarejea kufanyika kama hapo awali.

Aidha Dkt. amesema tangu hapo jana zoezi la uokoaji linaendelea vizuri na kikubwa zaidi uokoaji unaofanywa ni wa uangalifu na wenye ufanisi mkubwa ili kuweza kunusuru wahanga waliokwama kwenye ajali hiyo