Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

SERIKALI KUENDELEA KUWEKA MIPANGO YA KUSAIDIA KURASIMISHA BIASHARA ZA WAJASIRIAMALI WADOGO NA WAKATI


Chuo cha Elimu ya Biashara kuendelea kufanya utafiti wa namna ya kuwasaidie wafanyabiashara wadogo kusajili biashara zao kwa njia rahisi na inayomvutia kila anayetaka kuanzisha huduma hizo katika jamii.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo(Mb) Februari 16, 2026 chuoni CBE, Dar es Salaam, kwa lengo la kujionea utendaji wa kazi na kuzungumza na mejimenti ya Chuo hicho.

Pia Naibu Waziri alikipongeza chuo hicho kwa kuendelea kuongeza idadi ya machapisho ya kitaaluma akisema kuwa kufanya hivyo kunazidi kukiongezea hadhi chuo hicho kitaifa na kimataifa.