Habari
BALOZI SALUM: WATUMISHI WAWE WASAIDIZI WA BIASHARA, SI VIKWAZO
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda na Biashara, Balozi Waziri Salum ametoa rai kwa watumishi wa wizara hiyo na taasisi zinazosimamia biashara wasiwe vikwazo bali wawezeshe biashara kuzalishwa kwa wingi.
Aidha amewataka wafanyakazi katika wizara hiyo kufanya kazi kwa weledi na utu, wachape kazi na kubadilika kwani Rais wa Jamhuri ya Muunvano wa Tanzania Mhe. Dkt.Samia Suluhu Hassan anahimiza uwwkezaji wa viwanda nchini Tanzania.
Balozi salum ametoa rai hiyo baada wakati wa ziara yake katika Shirika la Utafiti na Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO) , Februari 19,2026 Jijini Dar es Salaam.
“Tusimame pamoja, tufanye kazi, biashara ifanyike, viwanda vijengwe vya kutosha,” amesema.
Amesema wizara inapaswa kutoka kwenye udhibiti na kwenda kuwezesha biashara ili watanzania wanufaike waweze kutengeneza maendeleo yao.
“Serikali kama hatuwezi kuwapa mtaji, tutengeneze mazingira ya unafuu kwa wabunifu,” amesema.
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu (TIRDO), Profesa Mkumbukwa Mtambo, amesema amepokea maelekezo yote hivyo watayafanyia kazi kwa kuhakikisha watanzania wanafahamu shughuli zinazofanyika katika shirika hilo kupitia vijana wabunifu.
