Habari
SERIKALI YATOA MAPENDEKEZO YA MIKAKATI YA KUKUZA BIASHARA NDANI YA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Serikali yatoa mapendekezo ya mikakati na mbinu za kukuza fursa na kuongeza kiwango cha biashara ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Hayo yamebainishwa na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Dennis Londo (Mb) wakati akiwasilisha taarifa kwenye Mkutano wa Kikanda wa ngazi ya juu wa wadau mtambuka unaojadili masuala yanayoathiri Biashara katika Jumuiya ya Afrika Mashariki Februari 20, 2026 jijini Kigali, Rwanda.
Mkutano huo umewakutanisha kwa pamoja wawakilishi wa sekta za Umma, sekta binafsi, asasi za kiraia na wanazuoni kutoka nchi wanachama, taasisi na vyombo ya EAC pamoja na wabia wa maendeleo kwa lengo la kujadili changamoto zinazoathiri kasi ya ukuaji wa biashara ndani ya Jumuiya na fursa zilizopo.
