Tanzania emblem
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Wizara ya Viwanda na Biashara

Habari

Dkt.Jafo aongoza harambee ya ujenzi wa Shile, Zaidi ya Mil.74 zapatikana.


v

Dkt.Jafo aongoza harambee ya ujenzi wa Shile, Zaidi ya Mil.74 zapatikana.

Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Dkt.Selemani Jafo (Mb) aongoza Wananchi wa Urambo katika harambee ya kuchangia ujenzi wa shule ya Bakwata katika Wilaya ya Urambo Mkoani Tabora.

Dkt.Jafo ameongoza harambee hiyo iliyosaidia kupata kiasi cha Tsh.Milioni 74,711,700 alipomwakilisha Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa(Mb), Oktoba 15,2024.

Katika harambee hiyo Viongozi mbalimbali wakiongozwa na Mbunge wa Urambo Mhe. margaret Sitta ,Mkuu wa Wilaya Mhe.Dkt.Khamis Mkanachi, Mkurugenzi,Viongozi wa Serikali na Dini mbalimbali, wananchi na wadau walichangia michango hiyo.

Aidha Dkt.Jafo amewapongeza Viongozi na Wananchi wa Wilaya ya hiyo kwa umoja wao katika kushirikiana kwenye mambo ya maendeleo.

Dkt.Jafo amesema amefurahishwa kuona umoja uliopo baina ya wananchi na viongozi wa Serikali na wa dini mbalimbali zilizopo Wilayani hapo hasa katika maendeleo hususani katika harambee ya ujenzi wa shule hiyo.

Vilevile Dkt.Jafo ametoa rai kwa Watanzania kujijengea tabia ya kuchangia shughuli za maendeleo kwa jamii kwani kutoa ni ibada na kunarahisisha maendeleo .

Mradi wa Shule hiyo kubwa na ya kisasa utagharimu fedha za Kianzania kiasi cha Sh. Bilioni 1 mpaka kukamilika kwake.